Friday, September 28, 2012

GOLDIE WA BBA APATA SHAVU LA KUFANYA KOLABO NA KERI HILSON MWAKA HUU.


Staa wa Nigeria ambae aliiwakilisha nchi yake kwenye shindano la Big Brother Africa 2012 Goldie ameongea na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kuamplfy kwamba kabla mwaka huu haujamalizika sauti yake na ya Keri hilson zitasikika juu ya beat moja na kuonekana kwenye video moja.

Ikiwa tayari Goldie ameshakuja Tanzania na kumaliza kurekodi kolabo yake na Ay inaitwa ‘Skibobo” amesema Mpaka sasa Keri Hilson amekubali kuifanya hiyo kolabo bure ambapo yeye Goldie atasafiri kwenda Marekani ndani ya wiki mbili zijazo na atakwenda kufanya mazungumzo ya mwisho mwisho kabla ya kuirekodi hiyo kolabo November au december 2012.

Mbalina hilo,Goldie  amesema mwanzoni alikua amepanga kufanya kolabo na Chris Brown lakini mawazo yakabadilika na sasa amefikia karibu kumaliza mazungumzo na staa mwingine wa kiume wa Marekani ambae hajapenda kumtaja.

Kasema tu kwamba huyo staa anaimba kama Chris Brown, yani wanafanya muziki wa aina moja lakini tofauti yake ni kwamba Chris Brown anaimba na kucheza sana ila huyo staa mwingine yeye hachezi, huwa anaimba tu, unaweza kukisia atakua nani? kama ndio nipe comment yako mtu wangu wa nguvu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!