Tuesday, September 18, 2012

HAFSA KAZINJA APEWA SHAVU NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI


Hafsa Kazinja akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bi. Mwanaidi Maajar
Mwanamuziki wa kike nchini Tanzania aliyewahi kutamba na wimbo ‘Pressure’ aliomshirikisha Banana Zorro, Hafsa Kazinja, yupo ziarani nchini Marekani.

Katika ziara hiyo, Hafsa Kazinja amepata bahati ya kutumbuiza mbele ya watu wa heshima nchini Marekani akiwemo balozi wa Tanzania nchini humo Bi. Mwanaidi Maajar.

Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza kwenye show kubwa Jumamosi ijayo, September 22, 2012.

Kwa upande wake mratibu wa show hiyo ambaye ndiye aliyempeleka Linah na Diamond nchini Marekani, Peter Ligate, amemsifia balozi Maajar kwa ukarimu wake na kuunga mkono shughuli za burudani.

“I must say our ambassador Maajar is an outstanding classic lady who is doing things that we have never seen our embassy do since I got 2 the US. We all should rally behind & support her 100% bless u mama balozi,” Ligate alisema kwenye maelezo yake.
Hafsa Kazinja akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali akiwemo Balozi Majaar
Hafsa akiwa na miongoni mwa wenyeji wake nchini Marekani, Missy Temeke
Hafsa, Missy Temeke na madansa watatu wa Diamond waliobaki nchini Marekani
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!