Thursday, September 20, 2012

HATIMAYE PICHA YA PREZZO NA GOLDIE AKIWA JIJINI NAIROBI YASAMBAA MITANDAONI
Hivi karibuni kituo cha Channel O kilikuwa jijini Nairobi kikiwa na mastaa kibao wa Afrika na kurekodi O News kwenye ukumbi wa KICC. 


Mastaa hao ni pamoja na Channel O VJs Denrele wa Nigeria, Jokate, J Town wa Ghana na Flavia wa Uganda.
Kulikuwepo pia na wasanii kama Khuli Chana wa Afrika Kusini, Banky W wa Nigeria na Wizkid.

Lakini pia kulikuwepo na ujio wa Goldie ambaye alienda kimya kimya. 

Kuna picha ilisambaa wiki hii inayomuonesha msichana mwenye nywele kama za Goldie akiwa na Prezzo japo sura haikuwa inaoenaka. 

Sasa kumepatikana picha inayowaonesha vizuri mastaa hao na kuthibitisha tetesi hizo huku ikionesha kuwa wapenzi hao wa BBA wanaelewana vizuri kwa sasa
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!