Saturday, September 15, 2012

HAYA NDO MASWALI TULIYOMUULIZA BANZA STONE KUHUSIANA NA SABABU ZA KUWAZA KUFA NA KUTUNGA NYIMBO ZA MWISHOHivi karibuni Banza Stone amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amekata tamaa ya kuishi na amekuwa akiota ndoto za kufa. 

Alisema kuwa yupo kwenye mpango wa kutoa nyimbo zake za mwisho kabla Mungu hajamchukua rasmi.

Mwandishi  aliamua kumtafuta Banza kwa simu ili kufanya naye mahojiano ya kina kuhusiana na jambo hilo.

Haikuwa rahisi kumpata kwakuwa simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Baadaye ilikuja kupokelewa na Banza kusikika akiongea Kiingereza muda wote na akisikika kama tayari kichwani alikuwa amechangamka kwa bia mbili tatu. 

Baada ya kupokea simu ndipo alipodai kuwa tumpe dakika mbili kwanza ajiandae. 

Baada ya kukamilika muda aliotaka tumpe ndipo mahojiano yalipoanza kama ifuatavyo:


Mwandishi: Naona Kiingereza kingi sana sasa hivi mzee imekuaje?
Banza: Ukiona hivyo ni elimu tu. Elimu ya mjinga ni majungu.

Mwandishi: Sasa hii issue ya kuota ndoto vipi imekuaje?
Banza: Ebana kila siku mwenyezi Mungu ana makusudi yake. Na makususi ya Mungu huenda ikawa labda ana nia yake ya kufanya kwamba jambo fulani linaweza kuwa ni sahihi. 

Maybe it’s not true, so otherwise we have to believe katika hili jambo ambalo linaweza likatokea pasipo kuwa na sababu, but me I believe God as a God……You know God about anything because God as a God, so otherwise mimi nabelieve sana God. 

Mwandishi: Okay, ndoto zikoje, unaotaje usiku?
Banza: Nasema hivi ndoto ni kitu ambacho cha mawazo, yaani unapokiwazia kitu fulani…. Pasipokuwa na mawazo maana yake wewe ni binadamu ambaye hujakamilika. 

So otherwise mimi hapa huenda ikawa nilikuwa katika mawazo fulani pasi mimi mwenyewe kujua kwamba kile kitu fulani, kinaweza kuwa ni kitu fulani but me, mimi naamini sana ndoto lakini si sana kivile kwasababu ndoto huenda ikawa ni kweli ama si kweli, isipokuwa uwe na imani katika vitu vyote viwili, ndoto zingine zinaweza kuwa za ukweli ndoto zingine zinaweza kuwa za uongo lakini you have to ‘choice’ about ndoto and ndoto so otherwise me nipo dillema, you know dillema? (anauliza). 

Yeah exactly, so otherwise mimi hapa nimebaki dillema tu but mimi nasubiri kile chochote kitakachotokea, it’s up to Mungu, it’s up to me.

 Mwandishi: Banza hebu muambie msomaji, ni ndoto gani ambazo unaziota

Banza: Nilihisi kama vile nakufa hivi! Lakini Mungu wakati mimi naota nakufa akaniambia bwana siwezi kufa sasa hivi. Lazima uwaachie ujumbe na ule umati ambao unakutegemea wewe katika maisha yako, meseji zako hazijaisha katika kuwapelekea wale meseji ambao wanakuzunguka, so otherwise you have to do uwapelekee meseji zao, zikishaisha wewe naweza nikakuhitaji, nikahisi kitu kama hicho yaani hiyo ni ndoto.

Baada ya kuwapelekea zile ndoto zako basi wewe ntakuhitaji lakini nikamwambia Mungu, (mawazo yangu) nikamwambia Mungu niache mimi kidogo niwape meseji zangu zitimie halafu wewe ukinichukua mimi ntakuwa nipo radhi katika kunichukua wewe lakini mimi namwambia hivi, Mungu niachie nafasi kidogo sababu nina imani kabisa kwamba meseji zangu bado hazijafika katika sehemu husika.

 Nina imani kuwa Mungu amepokea hili wazo, sababu Mungu ndio ‘mtu’ ambaye anaweza akapokea ombi la kila mwanadamu kwasababu sisi hapa tuko chini ya jua so otherwise Mungu lazima atuchukue sisi waja wake. Sisi tumekuja na lazima tuondoke. 

Kwahivyo Mungu pindi atakaponihitaji nitakuwa niko tayari. Na pindi Mungu atakapohitaji mimi niendelee kuwepo pia nitamkubali ili kusudi nipeleke meseji zangu ziwafikie, zikishawafikia, Mungu akinitaji, I am Okay.

Mwandishi: Unazungumza meseji, meseji gani ambazo unafikiria unataka uzipeleke kwa wasikilizaji?

Banza: Swali rahisi lakini swali gumu. Mimi nataka niwaambie hivi aliyekuwa anamtambua Banza kama Banza na yule ambaye alikuwa hamtambui Banza kama Banza, tena mimi nataka nielezee kwa wale ambao walikuwa hawamtambui Banza, nataka niwaachie meseji yangu kwamba wapate kumtambua Banza kwamba nini alichokifanya, nini anachokifanya na nini anachotarajia kukifanya.

Pale Mungu atakapompenda niwe nimeshakamilisha yale ambayo Mungu amenileta hapa duniani ili niwapelekee wale meseji watu ambao wapo hapa chini ya jua wapate kutambua kwamba Banza ameletwa duniani kwaajili ya kufanya kitu fulani. Sihitaji wale watu wapotee pasipokujua kwamba Banza amefanya kitu gani. 

Mimi nahitaji wale watu wapotee wangali wakijua kwamba Banza anaondoka alifanya kitu fulani ili kusudi kumbukumbu zao zibakie pale ya kwamba Banza alifanya kitu fulani, niwe ndani ya kumbukumbu zao za maisha yao na kila kitu kwao. Hata kama nitaondoka bado kumbukumbu yangu iendelee kuwepo. 

Mwandishi: Kwahiyo umeshaingia studio kurekodi hizo meseji unazozisema katika wimbo, upo katika taratibu za utunzi ama upo katika mkakati gani sasa hivi?

Banza: Kwa kifupi masuala ya utunzi binafsi yameshatimia ya kuzungumzia masuala haya ambayo ninayo. Isipokuwa binafsi yangu mimi naomba wale ambao wanamjua Banza waweze kumpa support aweze kufanya jambo hili japokuwa ni gumu. 

Hili ni jambo gumu sana la binadamu wenzangu kumpa support Banza aweze kuzungumza maisha yake, huenda ikawa anaweza akasita kwamba ahhhhh, nikimpa support Banza kesho atakufa lakini Mungu ndio mpanga wa kila jambo.

 Isipokuwa mimi nawaomba tu kwa nafsi yangu na kwa roho yangu na kwa kila kitu ambacho ninacho mimi hapa Mungu ambacho amenijalia, ninachowaomba wanipe support niweze kufanya hili jambo langu ili kesho kusiwe na maswali mengine ya kuhusu kwamba Banza alikuwa hivi ama alikuwa vile, niweze kuelezea mawazo yangu ambayo ninayo mimi hapa kabla Mungu hajanipenda.

Mungu akinipenda ntakuwa nimeshaacha wanavyosema wahenga nishaacha usia. 

Mimi naomba hivi yeyote mwenye kunisupport mimi kama Banza namkaribisha na namba yangu ni 0713 49 41 29.

  Yeyote mwenye kuhitaji kunigea support mimi hapa nikatengeneza albam yangu, siwezi kusema kwamba ni albam yangu ya mwisho, isipokuwa ni albam yangu ambayo nahitaji kuelezea maisha yangu ya mwisho, sina imani kwamba ni albam yangu ya mwisho.

Mwandishi: Mwisho unaweza ukatupa kionjo kidogo tu cha baadhi ya nyimbo ambazo umeziandika zenye ujumbe huu unaotaka kuufikisha?

Banza: (akiimba) Ndivyo nilivyo mimi Banza Stone, ndivyo nilivyo mimi miaka ohh! Sijui kosa gani nililokufanyia, naomba unieleze ule ukweli vile mimi kama nimekukosea naomba unisamehe, haya maisha sisi sote tunapita, sote ni waja wa Mungu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!