Wednesday, September 12, 2012

HII NDIYO "BONGO MOVIE STAR SEARCH" YA TINO NA KANUMBANadhani  sote  tunakumbuka yale mashindano ya kusaka vipaji vipya vya Bongo Movies yaliyokuwa yafanyike chini ya Marehemu Kanumba  lakini bahati mbaya  mauti ikamkuta.

Baada ya kifo cha The Great,  star wa filamu ya “Shoga Yangu” ambaye alikuwa partner in that idea is here to introduce to us the called “Bongo Movie Star Search“.


Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kuwa Tino, ambaye  jina lake halisi  ni Hisan Muya amaemua kuandaa shindano hilo baada ya familia ya Kanumba kuzuia kumpa documents za movie idol ambayo yeye na marehemu walikubaliana kuifanya.

“Ni kweli nimeamua kuanzisha shindano langu la Bongo Movie Star Search ili kusahka vipaji vipya kwenye sekta ya uigizaji nchini ambayo ita-cover almost mikoa yote ya Tanzania“.

“Nilienda kwa mzazi wa Steven Kanumba nikamwonyesha ushahidi wa kutosha kuwa mimi ninahusika kabisa kwenye mchakato ili nipewe kibali cha ku-organise search ile but waliniona kama mwizi wa idea, so kukwepa maneno nilishaenda kusajili shindano langu kwenye vyombo husika na tayari kibali cha kuendelea ninacho mwezi ujao naanza mchakato“, alifunguka Tino.

Alipoulizwa kama  ni copy and paste ya BSS ,Tino alikuwa na  haya ya kusema, “Kwani kuna ubaya gani nikafanya kitu kinachofanana na BSS kwenye maisha kuna kutegemeana, so sikuona tabu kuchukua ideas kwa Madam Ritha.Kikubwa ni sponsor aelewe“.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!