Wednesday, September 19, 2012

HII NDO KAULI YA MWISHO YA ORIJINO KOMEDI KUHUSU HALI YA VENGU


Nafaham ni watanzania wengi ambao wanalo hili swali kama mimi, toka tulipoacha kumuona msanii/mchekeshaji Vengu kwenye ORIJINO KOMEDI baada ya kuumwa, zilizuka stori nyingi sana lakini stori ya mwisho mimi kuipata ni kwamba alisharudi Tanzania akitokea kwenye matibabu India na afya yake inaendelea vizuri.

Baada ya kufahamu hivyo nikawa na kiu ya kutaka kujua ni lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani ya Orijino Komedi hivyo nikapata nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae ndio mkurugenzi wa kampuni inayoisimamia Orijino Komedi.

Namkariri akisema “ukweli niwe muwazi, kwa afya yake na tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, tunazungumzia kitu kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua muda mrefu sana ukizungumza ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni unakua unajidanganya wewe na watanzania wenzio, ndio maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea mtu unaempenda muombee, mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au mwaka ujao”

Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema “tutaendelea kuwa na jina la Vengu maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko tofauti kidogo sisi tumeapa.. ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa.. kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini tutaendelea kuwa saba, hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!