Monday, September 10, 2012

HII NDO PATASHIKA YA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 MKOANI SINGIDA USIKU HUU


Mtangazi wa Clouds Fm kupitia kipindi cha michezo Sports Extra Shaffih Dauda akisoma jina la mshindi wa piki piki inayotolewa na kampuni ya Push Mobile,kwenye mchakato mzima wa tamasha hilo,shoto kwake ni Mbwiga Mbwiguke ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha michezo na kulia ni Adam Mchovu akishuhudia tukio hilo usiku.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu ndani ya viwanja vya Singida Motel.
Mkali wa muziki wa bongofleva,Sir Juma Nature akiwakuna vilivyo wakazi wa Singida usiku huu kwenye tamasha la serengeti Fiesta 2012.
Mkali mwingine katika miondoko ya mitindo huru,ki-hip hop,Godzilla akikamua vilivyo jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mmoja wa wasanii wanakuja juu katika anga ya muziki wa bongofleva,Shetta akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Singida na vitongoji vyake waliofika kushangweka vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii Stamina,akiimba kwa hisia jukwaani mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Singida na vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya viwanja vya Singida Motel.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Ni Kushangweka tu ndani ya viwanja vya Singida Motel usiku huu
Rich Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye tamasha hili.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku huu.

Pichani juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo.
Baadhi ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta wakishangilia jambo.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mabeste na msanii mwenzake wakitumbuiza jukwaani usiku huu
Pichani ni Ofisa Mahusiano wa kampuni  Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B


Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.
Pichani kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!