Monday, September 10, 2012

HII NDO VIDEO MPYA YA 50 CENT


Wengi wanaamini 50 Cent amesahaulika kwenye muziki baada ya kupotezwa na Rick Ross, wengine wanaamini time ya 50 Cent imeshapita, wengine wanaamini labda ni kazi za Umoja wa mataifa anazodili nazo pamoja na biashara zake nyingine ndio hazimpi time ya kufanya sana muziki, na wengine wanaamini labda lebo yake ndio imechangia kwa sababu haikumpa sana support wala kuruhusu nyimbo zake mpya kutoka kama alivyotaka.

Hayo yote yanaweza yakawa maswali pia, lakini la msingi ni kwamba kama wewe ni fan wa 50 na umekua na kiu ya kusikia au kuona mziki wake mpya, time ndio hii..

 mchek kwenye video yake mpya hapo chini iliyotoka siku 6 zilizopita lakini mpaka sasa imetazamwa na watu zaidi ya laki 7 ambapo zaidi ya elfu 8 wameipenda na wengine zaidi ya mia tatu wameikataa kwenye Youtube….
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!