Friday, September 14, 2012

HIKI NDO KITUKO KILICHOIKUTA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.

Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana

Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.

Imekua ngumu kuwapata wahusika lakini mpekuziblog inaendelea kuwatafuta ili kujua mazingira ya wizi na kama kuna ushahidi wowote uliopotea pamoja na mambo mengine
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!