Sunday, September 16, 2012

HILI NDO TAMKO LA DIAMOND BAADA YA KUDAI KUCHAFULIWA NA GAZETI LA RISASI


Majina ya Diamond na Wema yameshakuwa kama wimbo wa taifa katika magazeti maarufu kama ya udaku hapa Tanzania. 

Ikiwa ni wiki moja tu tangu Diamond afanye show huko Malindi nchini Kenya, Jana Jumamosi september 15, 2012 gazeti la Risasi katika front page lilitoa story mpya inayomhusu Diamond, kuwa ana mahusiano mapya ya kimapenzi na binti kutoka Kenya na kichwa cha habari ni kama kinavyoonekana katika picha ya gazeti hilo hapo juu "WEMA, JOKATE MLIE TU!, DIAMOND ANASWA NA DEMU MPYAAA, Ni raia wa Kenya yadaiwa wana mipango mikubwa".

Leo Jumapili september 16, 2012 Diamond ameamua kuvunja ukimya kwa kutoa tamko lake kuhusiana na issue hiyo kupitia mtandao wake wa www.thisisdiamond.com. Na hiki ndicho alichokiandika:

 "Kiukweli nimesikitishwa sana na taarifa za mwanadada huyu kujinadi kua anamahusiano na mimi ya kimamapenzi na eti tunamipango mingi ikiwemo ya harusi ndani yake...

  Nimejiskia vibaya sana Kwani taarifa azitoazo msichana huyo si za kweli kabisa, Nilikutana nae Malindi akiwa kama mmoja ya Waandaaji wa tamasha hilo nililokwenda kutumbuiza na mbali ya hayo pia alikua ni mdogo wa Mwenyeji wangu wa Malindi, hivyo nilikua nikimchukulia kama dada yangu kumbe mwenzangu alikua anamipango mingine...

Nahisi Ukarimu wangu kwake na kuwa nae huru kama mmoja ya wenyeji wangu umeniponza, badala yake anatumia picha tulizopiga nae kwa namana nyingine....

Ukweli ni kwamba MWANADADA HUYO SINA MAHUSIANO NAE YA KIMAPENZI KABISA.... MPENZI WANGU NAAMINI KILA MTU ANAMJUA.....".....Diamond
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!