Tuesday, September 25, 2012

"WATU HUTUCHUNGULIA NYETI ZETU TUKIWA JUKWAANI".....SHILOLE

STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema suala la kuripotiwa kuwa wanavaa utupu linasababishwa na baadhi ya watu wanaopenda kuwachungulia wasanii wanapokuwa jukwaani na kuwapiga picha.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Shilole amesema watu hao wanatabia ya kuwachungulia kwa chini huku ‘wakiwafotoa’ picha na ndiyo chanzo cha matatizo mengi ya skendo zinazopamba mitandaoni kila kukicha.


“Yaani hili nimelishuhudia kwa macho yangu mtu anakuchungulia kwa chinichini halafu akikuotea vizuri ndiyo madhara yanakuwa makubwa kama tulivyoona kwa baadhi ya mastaa,” alisema Shilole.SWALI:
Kwa  nini wasanii  mnavaa nguo fupi?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!