Friday, September 28, 2012

HUYU NDIO BILIONEA ALIEAHIDI PESA KWA MWANAUME ATAKAEMUOA MTOTO WAKE AMBAE NI MSAGAJI.


Mwana na baba
Kama wewe ni mwanaume na una sifa zinazotakiwa basi jitokeze kuzichukua dola za kimarekani milioni 65 zilizoahidiwa na bilionea wa HongKong Mr. Chao ambae atazitoa kwa mwanaume yeyote atakaejitokeza kumuoa binti yake ambae anashiriki mapenzi ya jinsia moja (msagaji) kwa miaka saba sasa hivi.

Mr Chao anasema hajali kama huyo mwanaume ni masikini au tajiri lakini anahitaji mwanaume mwenye moyo wa kweli na upendo na asiefata pesa ili amuoe binti yake ambae anaishi Ufaransa kwa sasa na kumsaidia kuachana na usagaji.
Huyu wa kushoto ndio mpenzi wa huyu binti wa bilionea.

Chao ambae ana umri wa miaka 76 anatajwa kuwa bilionea ambae hajawahi kuoa lakini anadaiwa kutembea na wanawake zaidi ya elfu 10, ana watoto watatu tu ambapo wa kwanza ndio huyo msagaji mwenye umri wa miaka 33

Binti huyo msagaji ni msomi aliesoma Manchester University na baba yake amesema sio kwamba anamuuza wala kumlazimisha kuolewa, ni pendekezo tu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!