Saturday, September 22, 2012

"SADAKA ILINIFANYA NIKIMBIE KANISA".....JINI KABULA


Mwigizaji wa filamu Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’  hivi  karibuni alidai kuwa siku za nyuma baada ya kuzongwa na matatizo aliamua kumrudia Mungu wake kwa kuokoka katika kanisa moja maeneo ya Mwenge akiamini kuwa anaenda kupata faraja lakini alichokutana nacho huko ikibidi kurudi katika kanisa lake la awali.

“Unajua kuna wakati mtu unapokabiliwa na mitihani unaangalia njia sahihi ya kutafuta utatuzi, kwa wakati huo njia sahihi kwangu niliamua kuokoka na kujiunga na kanisa moja Mwenge, sasa kilichonikimbiza ni pale Mchungaji aliposema Mungu atakubariki ukitoa fedha nyingi kama sadaka,” alisema Kabula.

Jini Kabula kutokana na mahubiri hayo ya kuhimiza sadaka kubwa kuwa ndio kigezo cha kupata Baraka aliona kumbe maskini wanaosali katika kanisa lile wanapoteza muda kwani hawezi kuokolewa kwa sababu ya sadaka zao kuwa ndongo, Kabula akaona ni bora kurudi katika dhehebu lake la Sabato.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!