Saturday, September 22, 2012

"KIMBELEMBELE INAELEZA WAZI JINSI NILIVYOUMIZWA KWA KUMPENDA STAA".....AMINI

MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva kutokana na nyimbo zake za mapenzi Amini ameuambia mtandao huu  kuwa ngoma mpya ya ‘Kimbelembele’ , inazungumzia namna alivyoumizwa na mahusiano hasa yale ya kutoka na mwenye jina na kuonekana yeye ni kimbelembele.

Ngoma hiyo kinazungumzia namna alivyoanza mapenzi pindi alipoingia kwenye tasnia ya muziki, ambapo baadhi ya mistari inasema kuwa
“Wiki ya kwanza nilimpenda mwenye jina na nilipomuita jina lake alikataa na wiki nyingine nikampenda mwenye jina ’shida’ na kulipa luku ikawa shida” ni moja ya ujume mzito unaopatikana ndani ya ngoma hiyo.

Kutokana na maneno hayo wimbo huo unaonesha wazi kuwa wiki ya kwanza alikuwa na mahusiano na msanii mwenzake ‘Linah’ na walikuja kuachana baada ya mwanadada huyo kujiona ni staa ambapo hali ilikuja kujitokeza kwa mara ya pili baada ya kuwa katika mahusiano na mtoto ambaye kwao kulikuwa na matizo makubwa naye hakudumu naye.Lakini kama wadau wa muziki huu wanakumbuka moja ya hits za mwanadada Linah ni
‘Angalau’, ambayo inazungumzia mapenzi kama haya, ambapo nayo inasema angalau sasa nina furaha kwani pindi alipokuwa na Amini alikuwa hana furaha yoyote katika mapenzi kitu ambacho naye ameamua kujibu mapigo.

Amini alisema kuwa ngoma hiyo anaamini itatoa ujumbe kwa wale waliyomtenda ingawa kwa upande wake hana tatizo nao hivyo anawaomba radhi kama itawagusa sana au kama watajisikia vibaya kwani alichokiimba ndicho kilichotokea katika mahusiano yake ya mapenzi.


Hata hivyo Amini aliongeza kuwa anajuta kuwa na kimbelembele cha kutaka kutoka na staa kwani hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kutoa ngoma hiyo na aliyemuandika anajulikana kwani awali alimpenda lakini kutokana na kusifiwa na watu anauwezo mkubwa wa kuimba na mrembo akajiona malkia.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!