Friday, September 14, 2012

JACK WAMAISHA PLUS APATA TENDA YA KUPIGA PICHA ZA UTUPU AFRIKA KUSINI
STAA wa Maisha Plus Season II, Jacqueline Dastan ‘Jack Maisha Plus’, hivi karibuni alipata shavu la kupiga picha za utupu tenda iliyomtaka aende Afrika Kusini baada ya kukutana na mawakala wa kazi hiyo Bongo.

Akipiga stori na Mpekuzi , Jack alisema alipigiwa simu na wakala ambaye makazi yake ni Sauz akamwambia kuna dili kwa warembo wa Bongo kupiga picha za utupu nchini humo ambazo baadaye hupelekwa kuuzwa nje na kulipwa pesa nzuri zaidi.

 “Wakala huyo alinieleza kuwa picha hizo zitaenda kupigiwa Afrika Kusini na ni lazima niwe na Viza ya kusafiria, ukweli sina Viza lakini niliona siwezi kupiga picha hizo kwa sababu katika soko ningekuta zimetua kwetu Bongo,”
alisema Jack.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!