Saturday, September 29, 2012

JAFFARAI CAR WASH INAANZA RASMI LEO IKIWA NI SIKU YAKE YA KUZALIWA


Msanii wa muda mrefu katika music industry ya bongo Jaffarai a.k.a mteule, ameamua kuinvest katika biashara nyingine mbali na muziki kwa kufungua sehemu ya kutoa huduma za kuosha magari pamoja na service nyingine ndogo ndogo za magari.

Leo jumamosi 29th Sept 2012 ndio siku ambayo Car wash ya Jaffarai inafunguliwa rasmi na kuanza kutoa huduma. Car wash hiyo ipo maeneo ya Mikocheni Oilcom opposite TMJ hospital Dar es salaam.

Sababu kubwa ya Jaffarai kuamua leo ndio iwe siku ya ufunguzi ni kutokana na kwamba leo ndio siku yake ya kuzaliwa so ameona ni jambo jema kusheherekea birthday yake sambamba na ufunguzi huo.

We wish you a happy birthday Jaffarai, na hongera sana kwa investment yako hiyo mpya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!