Friday, September 14, 2012

JAY-Z AAHIDI KUMCHANGIA FEDHA RAIS OBAMA KWA AJILI YA KAMPENI ZAKEUshkaji wa Jay-Z na rais Barack Obama wa Marekani utaendelea wiki ijayo, pale rapper huyo na mke wake Beyoncé Knowles watakapoendesha shughuli ya kuchangisha fedha kwenye ‘fundraising dinner’ katika klabu ya Jay, 40/40 ya Manhattan.

Gazeti la The New York Post limeripoti kuwa chakula hicho cha usiku kitaalika wageni 100 tu ambao watalipa dola 40,000 kwa tiketi.

Dinner hiyo ya Sept. 18, inadaiwa kuwa kituo cha mwisho cha kampeni ya Obama jijini New York kabla ya uchaguzi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!