Sunday, September 2, 2012

JOKATE AMPONDA SNURA KWA KUJIFANYA MPAMBE WA WEMA SEPETU


MWANAMITINDO maarufu nchini Jokate Mwengelo, amedai kuwa msanii Snura asijifanye kuwa ameacha urafiki na best yake wa karibu Wema Sepetu kwani awali alikuwa kama mpambe ambaye alisahau kufanya kazi zake kwa kushindwa kusoma alama za nyakati.

Snura
amefunguka hivi karibuni na kudai kuwa eti ameamua kuachana na Wema Sepetu kwa madai kuwa alikuwa anakosa muda wa kufanya kazi zake, na badala yake muda mwingi alikuwa akifanya biashara za Wema huku akiwa
kama amsimamizi, na kazi zake zikiwa hazifananikiwi na kusonga mbele.

Chini ni picha za Wema akiwa kwenye viwanja tofauti na shosti wake.
Wakiwa D.I.A kwenye mapokezi ya star wa filamu kutoka Nigeria, Omotola Jalade


Hapa wakiwa pamoja siku ya uzinduzi wa filamu ya ‘Super Star’


Jokate
alipotafutwa na mwandishi wa mtandao huu ili kutoa kauli yake juu ya Snura kuachana na best yake wa karibu Wema, alidai kuwa kikubwa alichoharibu Snura ni kujifanya mpambe kwani alishindwa kufanya ishu zake badala yake alijiona kama mpambe wa Wema kwa kumfuata kokote anapokuwa.

“Unajua Snura alikuwa kama mpambe wa Wema na alishindwa kusoma alama za nyakati na sasa anadai kuwa ameachana na Wema amepoteza muda kweli mi sioni kama atakuwa ni mkweli zaidi ya uongo alionao,”
alidai.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!