Monday, September 10, 2012

KALAPINA AJA NA FILAMU YA TUKIO LA DR ULIMBOKA


Rapper aliyepotea kwenye ramani ya muziki wa Tanzania, Kalapina, yupo kwenye hatua za mwisho za kuanza kushoot filamu yake itakayozungumzia tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dr. Steven Ulimboka.

Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Kalapina amedai kuwa kinachomkwamisha kwa sasa ni bajeti ya filamu hiyo.

Hata hivyo amesema amepewa ahadi ya shilingi milioni 3 kutoka Profesa Ibrahim Lipumba kusaidia kukamilisha maandalizi yake.

Amewataka wadau wengine wamuunge mkono kwakuwa anataka kuwaonesha watanzania utofauti katika filamu za Tanzania.

Amesema filamu nyingi za hapa nchini zimejikita katika visa vya kufikirika na mapenzi na yeye anakuja na filamu inayozungumzia tukio la kweli (based on a true story)

Ameongeza kuwa script ya filamu hiyo ipo tayari na wahusika wote katika filamu wameshapatikana.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!