Sunday, September 16, 2012

Khadija Mnoga aka KIMOBITEL AANZA KAZI EXTRA BONGO

Khadija Mnoga aka KIMOBITEL akiimba wimbo wake mpya "Mgeni" wakati wa utambulisho wake rasmi wa kujiunga na Bendi ya Extra Bongo ndani ya New White House Kimara Korogwe Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Kimobitel akiimba na Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la "Mgeni" ndani ya New White house wakati wa utambulisho wake rasmi.
Comredi Ally Choki aka Mzee wa Farasi
Kimobitel akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo wakati aliokuwa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa maeneo ya Sinza na maeneo ya jirani.
Makamanda wa Extra Bongo wakiongozwa na Ally Choki mwenye Tsheti nyeupe mbele, kutoka kushoto ni Banza Stoni, Kimobitel na mwisho kulia ni Rogert Hega aka Katapila wakiimba wimbo mpya wa Hadija Mnoga aka Kimobitel.
Ally Choki Mkurugenzi wa Extra Bongo akiimba kwa furaha wimbo wa "Mgeni" ulotungwa na Khadija Mnoga (Kimobitel). Mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) wiki iliyopita alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa Habari kujiunga na Bendi ya Extra Bongo akitokea bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) aliyoifanyia kazi kwa miezi kadhaa. Juzi Ijumaa na Jana Jumamosi ndiyo zilikuwa siku rasmi za kutambulishwa kwa mashabiki na wapenzi wa Extra Bongo
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!