Sunday, September 16, 2012

"ALLY KIBA NA MAMA YAKE WANAMAMBO YA KIJINGA SANA"......HILI NI TUSI LA TID


Baada ya kukabiliwa na scandal kubwa ya kupanga njama za kumuua Ali Kiba, Khalid Mohamed aka Top in Dar, amezungumza na kusema Ali Kiba na mama yake wamekosa la kufanya na anawaona wajinga wakubwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, msanii huyo amesema huenda Ali Kiba alienda kwa mganga ambaye alimwambia TID anataka kumuua.

Msanii huyo wa ‘Nyota Yangu’ aliongeza kuwa kutokana na kusingiziwa kitu asichokijua, kamwe haiwezi ikatokea siku atampigia tena simu Ali Kiba aliyekuwa mshikaji wake wa karibu.


“Siwezi naogopa,” alisema. “Naweza kumpigia simu nikaambiwa sasa ndo natamtafuta kumuua, achana naye tu mwache yeye aendelee na vitu vyake, because I felt he and his family were up to it, mama yake namuona sana, najua mama yake hanijui hajawahi kuniona hata siku moja.

 Ali Kiba kwa kitu gani ambacho amefanya yeye mimi nimfanyie baya? Nipo na watu kibao pale nao wamejilist eti nataka kuwaua sasa mimi hela ngapi nitatoa kuwaua watu wote wale? For what purpose watu kibao wamejilist. 

Am not gonna tell you what reactions I’m gonna do, I’m keeping it to myself, I aint gonna talk about it, seriously they are stupid, yaani they should come up with the best concept.”

Pia Top In Dar alisema ameshakutana na Diamond ambaye amesema hata haelewi kinachoondelea na hana tatizo naye.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!