Wednesday, September 26, 2012

LENNAH NDIO QUEEN MPYA WA DANCEHALL TOKA OGOPA


Lennah ni msanii mpya ambaye amejipatia  mashabiki wengi ndani ya music scene nchini Kenya. Msanii huyu wa kike mwenye umri wa miaka 20 ameweza kurecord single yake ya kwanza kwa jina la “Fairness of My Heart,” chini ya Ogopa DJs.

Lennah ni mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha kiitwacho Inoorero ambaya ameanza kuimba akiwa na umri  mdogo, but ana ndotoza kuja kuwa moja ya Superstars kwenye upande wa music nchini Kenya na ameshaperform kwenye festival nyingi akiwa na wanafunzi wenzake.

Msanii huyu ameweza kutoka kwenye game baada ya kusaidiwa na manager wake mpya kwa jina la Solexx na sasa yupo studio akitengeneza track yake ya pili ambayo amemshirikisha K-daddy.

Hapa chini ni Single ya Lennah kwa jina Fairness of My Heart:

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!