Friday, September 14, 2012

MAMBO MATANO USIYOYAFAHAMU KUHUSU MAISHA YA JINI KABULAKatika kipindi cha wiki hii  cha Take One cha Clouds TV, muigizaji wa filamu aliyejiiingiza kwenye muziki hivi karibuni na mwenye scandal kibao nchini, Miriam Jolwa, ameweka hadharani masuala ya ndani kabisa ya maisha yake ambayo wengi walikuwa hawayafahamu. Mambo hayo matano ni kama ifuatavyo.

1. Uhusiano alionao sasa na mzazi mwenzie Tuesday Kihangala aka Mr. Chuzi

Kwanza nimzungumzie chuzi kama Chuzi, kama mzazi mwenzangu kama bosi wangu, najivunia sana kufanya kazi na Mr. Chuzi ni mtu ambaye ananiwezea kikazi, ni mtu ambaye ananipenda yaani. Unajua ni wachache sana ambao wamezaa sijui halafu bado muendelee kuwa pamoja. 

Ukiona mtu umezaa naye halafu hakumfunga ndoa halafu mko karibu ujue yaani huyo mtu anampenda yaani bado ananipenda, bado ananihitaji, naye anajivunia mimi kuwa Jini Kabula kuwa na mtoto wake. 

Kwahiyo najivunia sana kufanya kazi na Mr. Chuzi. Sina uhusiano naye, ndo maana alipotoka Jini Kabula akaja Jack wa Chuzi, akaja Rose wa Chuzi sijui akaja nani na atakuja mwingine wa Chuzi, ila mimi tupo kikazi tu.

2. Tukio analolichukia maisha mwake
Kuna kipindi nilipotea sana nilikuwa mlevi kupindukia, kwahiyo ni kitu ambacho kilinishusha katika jamii. Yaani ni tukio ambalo nikikumbuka naanza kujiona nilikuwa mjinga, kwasababu stress hazimaliziki….yaani hazimalizwi kwa pombe. Kwahiyo nikawa mlevi kupindukia , yaani ilikuwa kila ukinikuta Kabula yuko bwiiiii! 

Yaani hata ile thamani yangu ya ustaa ikawa inashuka sasa., lakini nashukuru watu wazima waliniweka chini wakanielewesha na nikaacha hicho kitu.

3. Tukio analolifurahia maishani mwake
Najivunia sana kuitwa mama, ndio tukio ambalo nalifurahia katika maisha yangu. 

Yaani siku niliyotoka labour, nikaenda mimi labour kama mwanamke, kama Miriam Jolwa halafu nikatoka nikasikia kichanga kinalia yaani halafu nikaanza kukiweka hapa kitoto changu kukinyonyesha mpaka leo kina miaka minne, yaani ni tukio ambalo nalifurahia sana kwasababu sikuamini, sikujua kama mimi nina uzazi.

Nilikuwa najiona tu mimi kama mimi lakini mpaka nikabeba ujauzito mwenyezi Mungu akanijalia nikaingia labour nikajifungua salama mtoto wangu yupo anaishi, yaani ni tukio ambalo nalipenda sana katka maisha yangu. Anaitwa Salma.

4. Sababu za kwenda kufanya fujo nyumbani kwa Mr. Chuzi
Sikuwa nafanya fujo, nilienda kumchukua mtoto wangu kama mama, baada ya kuona mtoto yaani malezi anayoyapata hayaendani na yeye. 

Sababu yule Chuzi ni baba, baba anahangaikia familia, siwezi kusema eti Chuzi akae nyumbani amlee mtoto, yeye ni mhangaikaji, anahangaikia familia, labda kwa huyo mwanamke aliyekuwa naye anaact. Chuzi akiwepo nyumbani yaani akawa sasa kama anacheza movie. 

Chuzi akiwepo nyumbani anaonesha upendo kwa mtoto, lakini Chuzi akitoka mtoto……. Sasa mimi nikawa naambiwa, shangazi zake, housegirl ananiambia dada hivi na hivi.
Na kweli siku nimeenda nikamwangalia mtoto wangu nikakuta afya yake iko tofauti na kipindi cha nyuma nilipokwenda kumwangalia. 

Yaani nikamkuta yuko tofauti, nilichosema mimi namtaka mtoto wangu, yeye akawa hataki, nikamwambia kama hutaki basi kuwa houseboy, usifanye kazi lea mwanao ama panda naye kwenye gari lako uwe unaenda naye unarudi naye.
Sasa ikawa imetokea pale mtafaruku kidogo mimi nikamchukua mtoto wangu kwasababu uchungu wa mtoto aujuaye ni mama, yeye ni baba tu. 

Nikaamua nimchukue mtoto wangu nikampeleka kwa mdogo wangu ambaye ni mwanasheria yupo Kurasini. Baada ya hapo tukakaa kama watu wazima akanibembeleza, unajua Chuzi anampenda sana mtoto wake. 

Baada ya kunibembeleza sana, nikaona ngoja nimpe bwana, maisha yenyewe mafupi, acha nimpe akipendacho, ndo nikaamua kumrudishia mtoto lakini kwa masharti, na mpaka leo mtoto yuko poa. 

5. Kuhusu tetesi kuwa ana ujauzito wa Bushoke
Ni jambo la heri. Kama yapo yanayosemwa, hilo ni jambo la heri kwangu, kwasababu kuna wanawake wengi wanatafuta watoto na hawapati. 

Kama lipo, basi nashukuru Mungu, tumsubiri ‘Kijacho’. Baba yupo tu atajulikana kwasababu hakuna mtoto asiyekuwa na baba.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!