Sunday, September 9, 2012

MASHAIRI YA KANYE WEST KWENYE "KNOCK YOU DOWN" YALIMHUSU KIM KARDASHIAN

Kanye West hajaanza kumpenda Kim Kardashian juzi. Aliuweka wazi upendo wake kwa mrembo huyo tangu mwaka 2009 wakati (Kim) alipokuwa mpenzi wa Reggie Bush lakini hakuna aliyeweza kugundua.

Vyanzo vilivyo karibu na Yeezy vimeuambia mtandao waTMZ kuwa rapper huyo aliandika mashairi kuelezea upendo wake kwenye wimbo alioshirikishwa na Keri Hilson, "Knock You Down."

Mashairi yaliyomlenga Kim yalisema, "You was always the cheerleader of my dreams / To seem to only date the head of football teams / And I was the class clown that always kept you laughing / We were never meant to be, baby we just happened."

Aliongeza kwenye wimbo huyo kwa kusema , "You should leave your boyfriend now."

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!