Wednesday, September 26, 2012

"JAPOKUWA MIMBA YANGU IMETOKA,LAKINI NI LAZIMA NIZAE NA BUSHOKE".......JINI KABULA

MWIGIZAJI machachari Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya ujauzito wa awali kuharibika, bado ana nia ya kuzaa na mpenzi wake Rutta Maximilian Bushoke aliye mwanamuziki wa Bongo Fleva.

Akipiga stori na mpekuzi jijini Dar es Salaam,  Jini Kabula alisema bado ana hamu ya kuzaa na mpenzi wake huyo.


“Haikuwa riziki, ilikuwa bahati mbaya, dhumuni langu lilikuwa ni kuzaa na Bushoke kwa sababu nampenda, hivyo Mungu akinijalia tena, nitazaa naye tu. Natamani sana niwe mama wa mtoto wake,”
alisema Jini Kabula.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!