Friday, September 28, 2012

MISS DODOMA AWAPONDA WAREMBO WANAOKIMBILIA BONGO MOVIE....ASEMA SANAA HIYO IMEPOTEZA MUELEKEO


Aliyekuwa anashikilia taji la Miss Dodoma na Miss Kanda ya kati mwaka 2009 -2010 Jackline Nitwa amesema hana mpango wa kuingia katika tasnia ya filamu nchini kwa kile kinachodaiwa tasnia hiyo inapoteza muelekeo

Anadai kuwa tasnia hiyo imekuwa ikiingiliwa na baadhi ya warembo huku wakiwa na dhana ya kufanya vizuri wakati hawana hata muelekeo wa kipaji cha kuwa waigizaji na badala yake huingia huko na kuharibu tasnia hiyo


Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mikakati yake ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu alisema kuwa warembo wanafuatwa na waandaaji wa filamu kwa kigezo cha kuigiza lakini ndani yake wanakuwa na lengo lingine


“Mimi nimeshafuatwa sana na hao waandaaji lakini wanapokuja wanakuja na nia zao nyingine kama za kukutaka kimapenzi na kupoteza uhalisia wa kazi yenyewe, mimi siwezi kuingia katika tasnia hiyo “ alidai

Anasema kuwa hawezi kuingia katika tasnia hiyo kwani amejikita katika masomozaidi ili aweze kufanikiwa kwa kutumia elimu yake na iwe muongozo kwake.
 
Anadai kuwa ukiwa mrembo, jamii inakuzungumzia tofauti sana hivyo unatakiwa uishi kimaadili ili wanaokuiga waige mazuri kutoka kwao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!