Wednesday, September 5, 2012

MISS PROGRESS INTERNATIONAL APATA SHAVU MAREKANI

.

MISS Progress International 2010/11 anayechipukia kwenye filamu, Julieth William  amepata shavu nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa watu wanaosaidia wasiojiweza.


Akiongea  na mwandishi  wetu, Julieth alisema alipata mwaliko huo kutoka kwa shirika linaloshughulika na kusaidia wasiojiweza linalotambulika kwa jina la Humanity and Culture Values ambapo linafanya mkutano wa kitaifa nchini Marekani.


“Mwaliko huu nimeupata kutokana na mradi ninaouendesha wa kusaidia watu wasiojiweza na walemavu wa ngozi.  Nimefurahi sana kwani wameona umuhimu wangu,” alisema Julieth ambaye anatarajia kuondoka nchini Septemba 25, mwaka huu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!