Wednesday, September 26, 2012

"BONGO MOVIE NA BONGO FLEVA WOTE NI VICHECHE NA HATUPASWI KUCHEKANA".....HUU NI UJUMBE WA HUSNA KWA NEY


STAA wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ amemvaa mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ na kusema wimbo wake uliolenga kuwachafua Bongo Movies, ulipaswa uwe wa wanamuziki na si wao.

Akizungumza na mpekuzi, Sajent alisema amesikitishwa na wimbo wa Nay uitwao Nasema Nao ambao ndani yake kuna mashairi ya kuwaponda wasanii wa filamu kuwa ndiyo wanaoongoza kwa umalaya.

“Hata siku moja nyani hajawahi kuona makalio yake, yeye ataendelea kuwacheka wenzake kuwa wana makalio mekundu, lakini hajayaona yake.

“Ni sawa na Nay sasa. Yeye ni mropokaji, anatafuta njia ya kujipaisha kisanii. Sasa jamani, hivi sisi wa filamu na wao (Bongo Fleva)  ni akina nani wanaongoza kwa umalaya? Atasema sana, lakini ukweli utabaki palepale na huyo Nay mwenyewe anauja ukweli.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!