Monday, September 3, 2012

MREMBO WA KIMAREKANI "AJIGONGA" KWA AY BAADA YA WIMBO WAO KUTAJWA KUWANIA TUZO ZA CHANNEL O
Kila msanii popote pale duniani hufarijika pale wimbo wake ama alioshiriki unapokuwa nominated kuwania tuzo kubwa. Nominations zinaongeza uzito kwenye CV ama portfolio ya msanii. 


Hivyo habari ya video ya ‘Speak with your body’ ya Ambwene Yesaya kutajwa kuwania kwenye vipengele viwili (Most Gifted Male Video of the Year na Most Gifted Video of the Year) kwenye Channel O Music Awards 2012, si habari njema kwake tu, bali hata kwa wale walioshirikishwa.

Wengi walitaka kujua reaction ya Lamyia Good, mwanamuziki mrembo wa Kimarekani aliyeshirikishwa kwenye ngoma hiyo.

Kama tulivyosemwa mwanzo, nominations za tuzo kubwa ni habari njema kwa msanii yeyote, umjuaje! Soon as she heard the news, the sexy Lamyia went bananas! If AY was around near her, she would have jumped into AY’s arms and give him such a ‘passionate kiss’ as a sign that it was a great job! That’s what we always do when we are excited right? Baada ya kusikia habari hiyo njema, Lamyia akatweet: Wow congrats #teamnosleep AyTanzania @hemdee31 @RileyCEO @romeomiller on 3 channel O awards nominations! LET’S GO!!

“Yeeah!! Kamin to LA soon, can’t wait 2 team up with ma CREW,” alijibu AY.

“Yaaay! My AY!!! Yes #teamnosleep meeting at the bat cave soon as you get here! Lol,” alimalizia Lamyia.


Hivyo tunahisi hii ‘timu isiyolala’ ikikutana Los Angeles, California, pataangushwa party ya nguvu kupongezana na huenda hapo ndipo AY atapewa ‘kumbatio’ lake kutoka kwa Lamyia.

AY pia ametajwa kwenye kipengele cha tatu cha Most Gifted East African Video of the Year kwa wimbo wake aliowashirikisha Sauti Soul wa Kenya, I Don’t Want to Be Alone.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!