Wednesday, September 5, 2012

MSAADA KWA WANAOJIUZA: HUU NDO UZINDUZI WA NYIMBO ZA INJILI WA PASCHAL CASSIAN (BSS 2009) WENYE LENGO LA KUSAIDIA MAKAHABA UWANJA WA FISI

Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Ritha Paulsen (katikati) akikata utepe kuzindua albamu ya mshindi wa shindano la BSS 2009 Paschal Cassian (kulia).
Paschal Cassian akikamua vilivyo wakati wa uzinduzi wa albamu yake uliofanyika uwanja wa Fisi jijini Dar.
Mwimbaji Martha Mwaipaja nae alifika kumpa shavu Paschal.
Madam Rita akichangisha fedha za kwa ajili ya huduma ya kuwasaidia machangudoa wa Uwanja wa Fisi.

MSHINDI wa shindano la BSS 2009 Paschal Cassian amepania kukusanya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kupambana na biashara ya uuzaji wa miili inayofanywa na machangudoa wa uwanja wa Fisi.

Cassian alisema hayo wakati akizindua albamu yake ya nyimbo za injili iitwayo  Yasamehe Bure,  yenye nyimbo nane.
Nyimbo hizo ni  Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.


Kama ilivyo kawaida katika uzinduzi wa nyimbo za injili huwa kunakuwa na wakati wa kuchangisha fedha za kununulia albamu husika ambapo katika tukio hilo MC alianza kwa kuelezea uuhimu wa kuchangia albamu hiyo.


Mbali na kufafanua kwa inalenga kuwasaidia akinadada wanaojiuza lakini pia alisisitiza kuwa akinadada hao watapatiwa njia mbadala ya kuondokana na sakata hilo.


Naye Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) Ritha Paulsen aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alipopanda jukwaani alianza kwa kumkosoa MC kwa kusisitiza kuwa inatakiwa hata hao wanunuaji kwa maana ya wanaume kuacha kununua mara moja.


Alisema kuwa ili kupambana na biashara hiyo haramau inatakiwa kwanza wanaume kuepuka kwenda kununua madada hao kwa kuwa wanunuzi wasipokuwepo basi hata wauzaji hawatakuwepo.


Pia alichangia albamu hiyo kwa kuinunua kwa milioni 10 ili kufanikisha kampeni hiyo muhimu.


Naye Cassian alichangia kwa kusema kuwa akiwa kama kijana mbali na kumtumikia Mungu kwa kila jambo pia ameona kuwa ni wakati muafaka wa kuwatumikia wanadamu ambao ameanzia kwa wanadada hao wa Uwanja wa Fisi.


Uzinduzi huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu waliojitokeza katika eneo hilo huku wengine wakiwa wanaimba nae na kucheza nae pamoja.


Akizungumzia zaidi albamu hiyo alisema kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa kuwapatia ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!