Friday, September 14, 2012

MWANA FA AAMUA KUFUATA NYAYO ZA AY


Mwaka huu rapper kutoka Tanga yalipozaliwa mapenzi Hamis Mwinjuma aka Mwana FA, ameamua kufumba macho na kuingia kwenye akaunti yake kuchukua mkwanja mrefu ili kufanya video kali na za gharama kubwa kama za swahiba wake AY. 


Japo hatofanya video ya dola 20,000 kama ‘Party Zone’ ya AY, Mwana FA anatarajia kukata dola 8,000 kumlipa director wa video yake.

Kiasi hicho ni kile anachotakuwa kumlipa director tu na haijumuishi gharama zingine.


Amesema video atakayoifanya ni ya wimbo wake mpya aliowashirikisha Wyre na Prezzo alioupa jina na ‘Give Me That Song’ uliofanyika nchini Kenya.

Video hiyo itafanyika Nairobi, Kenya japo hakuitaja kampuni ama director atakayehusika.

Baada ya kupiga show kwenye fainali za Nokia Don’t Break The Beat jijini Nairobi na show za Fiesta, dola 8,000 si pesa ya kumpa mawazo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!