Monday, September 10, 2012

MWASITI APATA SHAVU LA KUFANYA NGOMA MPYA NA PRODUCER WA AKON

Mwanamuziki wa kike wa Bongo Flava Mwasiti amepata shavu la kufanya ngoma mbili na producer aliyewahi kutengeneza ngoma za Akon.

Producer huyo aitwaye Hakim Abdulsamad ndiye aliyeproduce ngoma kadhaa za Akon zikiwemo, Be With You, Mama Africa na Clap Again pamoja na kuhusika kutengeneza nyimbo za msanii mkongwe wa Senegal, Youssou N’dour.“Nafanya naye kazi mbili, kazi ambayo nimefanya naye ya kwanza ambayo yeye mwenyewe alikuwa hapa hapa ni ambayo inaitwa ‘Bwana Yake’ lakini wimbo wa pili ambao nimefanya naye ndio wa kwangu sasa wa kibongo flava zaidi,” Mwasiti aliiambia Top 20 ya Clouds FM.

Mwasiti alisema ‘Bwana Yake’ ni wimbo alioufanya kwaajili ya kuzungumzia ukatili wanaokutana nao wanawake kwenye jamii zetu.

Hakim ni producer wa Marekani ambaye alikuwa miongoni mwa ndugu waliounda kundi la R&B liitwalo The Boys lililoundwa na kaka zake wengine Khiry, Tajh na Bilal.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!