Friday, September 21, 2012

"JB NAYE NI KICHECHE KAMA WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL".......NEY WA MITEGOMsanii wa muziki  hapa  nchini, Ney wa Mitego jana amemuangushia bomu muigizaji wa filamu nchini, Jacob Steven aka JB kuwa hana tofauti na waigizaji wa Bongo Movies anaowachukulia kama vicheche.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye kipindi cha Hot Mix cha EATV baada ya hivi karibuni kukwaruzana na JB jijini Mwanza kwenye ziara ya Fiesta. Inadaiwa kuwa Ney alimwita Wema kicheche jukwaani jambo lililomfanya muigizaji huyo kukwaruzana na Ney.

“JB alikuwa kama mtoto mdogo au ulifika time wacha tu niliongee hili,” alisema Ney.

 Ilifika time nikasema JB simtofautishi na wale akina Aunty Ezekiel sijui akina Wema kwasababu unajua mtoto wa kike ni dhaifu unajua, mimi nilimsamehe Aunt Ezekiel na Wema pia, sababu Wema na Aunty Ezekiel ni watu waliotaka kugombana na mimi, niliwasamehe palepale.

 Nachokisema sio kama nabahatisha, nakuwa na uhakika nacho. JB na Ray ilibidi waungane pamoja wanifuate, ‘bwana unajua mimi ni dogo kwao’ lakini labda tunashindana tu vitu fulani, ukubwa wa umri si tatizo.”

Uhusiano mbaya kati ya waigizaji wa filamu nchini na Ney ulianza baada ya rapper huyo kudai kwenye wimbo wake‘Nasema Nao’ kuwa makahaba wenye kiwango wapo kwenye Bongo movies.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!