Monday, September 10, 2012

NICK MINAJ AMPIGA CHINI BARACK ABAMA......Ulimwengu wa hip hop ulipigwa na butwaa kufuatia tetesi kuwa Nicki Minaj ni mkereketwa wa chama cha Republican na atampigia kura mgombea wake wa urais Mitt Romney.

Tetesi hizo zilianza kuzagaa kutokana na mashairi yake kwenye wimbo alioshirikishwa na Lil Wayne uliopo kwenye mixtape yake mpya.

Mashairi hayo yaliyopelekea mpaka mashabiki kumtishia kumuua Nicki yalisema, “I’m a Republican voting for Mitt Romney, you lazy b****es is f***ing up the economy.”


Hata hivyo mtandao wa RumorFix umefanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa rapper huyo mwenye miaka 29 hawezi kupiga kura.

Kwa mujibu wa rekodi, rapper huyo anamiliki nyumba kwenye majimbo ya Georgia, California, na New York na anaruhusiwa kupiga kura kwenye jimbo lolote lakini tatizo ni kwamba hajajiandikisha.

RumorFix ilipiga simu kwenye ofisi za uandikishaji wapiga kura kwenye kila jimbo la kuthibitisha kuwa hakuna jina la Nicki Minaj ambaye jina lake halisi ni Onika Tanya Maraj.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!