Monday, September 10, 2012

NIGERIA WAZIDI KUWIKA BAADA YA J MARTINS NAYE KUREKODI KOLABO NA RAPPER PITBULL.


J.lo na Pitbull.
J Martins.
Mpaka sasa Nigeria inaongoza kwa idadi ya vijana wake kufanya kolabo na mastaa wa muziki wa dunia kutokea Marekani pamoja na kupata deals, mfano ni kwa kolabo waliyoifanya P Square na rapper Rick Ross pia kolabo yao na Akon lakini pia Dbanj ambae yuko chini ya lebo ya Kanye West.

Naomba kukufahamisha kwamba kolabo inayofata sasa hivi ni ya Producer/msanii J Martins ambapo tayari ameshairekodi na Cuban American Rapper Pitbull na mpaka sasa jina la kolabo yenyewe halijatajwa.

Kingine ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba wiki chache zijazo ndio video itafanyika kwenye mji wa Amsterdam ambapo stori kamili zinadai  kwamba ni hit ambayo Pitbull amelenga kupanua zaidi soko lake ambalo kwa sasa ni USA na Latin America na J Martins pia anataka kuvuka boda na kwenda umbali mrefu.

Bado haijawekwa wazi jamaa walikutanaje mpaka akakubaliwa kolabo lakini kolabo hiyo itamsogeza sana J Martins kwa sababu Pitbull ni staa ambae ameshine kwenye nyimbo zake na hata kolabo nyingi alizofanya na wakali kama J.Lo na Ne-yo.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!