Friday, September 14, 2012

NIKKI MBISHI AKANA KUMDISS LOVENESS LOVE KWENYE NGOMA YAKE IITWAYO FEEDBACK
Rapper anayeheshimika kwa uandishi mkali wa mashairi na mchawi wa freestyle Tanzania, Nikki Mbishi, amekanusha kumdiss mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Diva, katika wimbo wake uitwao ‘Feedback’ uliopo kwenye albam yake, Jogoo.

Mstari huo unasema, “Hauwezi kuiva mpaka uwe unamskiliza Loveness Love,Kicheche unajiita diva hiyo ni nonsense kavu.”


Hata hivyo akiongea na 255 ya Clouds FM jana, rapper huyo amesema mlengwa wa mstari huo sio mtangazaji huyo bali ni ex wake aliyemzingua.

“Huo mstari nilimchanaga mtu mmoja ambaye niliwahi kuwa na uhusiano naye akanizingua, halafu sehemu aliyokuwa anatumia kijifunza mapenzi ni kile kipindi cha Loveness Love, ndo maana nikamuuliza huwezi kuiva kimapenzi mpaka uwe unamsikiliza Diva? 

Umeona, kwahiyo yeye sasa mwisho wa siku ikafika hatua hadi anajiita diva, nikamwambia wewe ni kicheche unajiita diva? 

Halafu hiyo ni nonsense kavu yaani, sababu haina maana wala misingi yoyote katika uhusiano wangu mimi na wewe, ndo maana ya huo mstari, lakini haikuwa direct kwamba namchana Love sijui ni nini,hapana yeye hahusiki na wala hajui nini maana ya huo mstari yaani," alisema Nikki Mbishi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!