Tuesday, September 11, 2012

" NITAUTUMIA UBALOZI WA ONE CAMPAIN KUSAIDIA WENYE NJAA"....PREZZOMshindi wa pili wa Big Brother Africa Stargame, Jackson Makini aka Prezzo amesema kazi yake kama balozi wa One Campaign ni kukuza uelewa kuhusu balaa la njaa na matatizo yanayowakumba waafrika maskini na sio kwaajili ya kujinufaisha kiuchumi.

“Sisi tuko poa you know, tukitoka hapa tunaenda kupata zege but kuna sehemu yaani Afrika ambapo hawapati msosi kabisa,” Prezzo alisema kwenye kipindi cha Mkasi cha EATV kilichorushwa jana usiku.


Alisema anategemea kuanza majukumu yake kama balozi wa kampeni hiyo katikati ya mwezi huu ambapo ataripoti kwenye makao makuu ya One Campaign mjini Washington DC.

“Washington DC nitakaa kama wiki na nusu, orientation you know, wanipe bendera yangu ya gari, wanipe passport yangu.”

Alieleza kuwa akiwa Washington atatengeneza t-shirt zake alizozipa jina la ‘Swagga Farmer’ na ndipo atakapoelekea jijini New York kwenye show ya Jay-Z.

Prezzo aliongeza kwa kudai kuwa kama balozi wa One Campaign anataka kuona analeta mabadiliko fulani katika bara la Afrika na kama kampeni hiyo ikifanikiwa kupunguza njaa katika maeneo duni barani humu, atajipongeza.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!