Friday, September 14, 2012

"NIMEMUIMBIA OBAMA KWA MAPENZI YANGU"-DOKII


Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Ummy Winslaus alias ‘Dokii amesema kuwa wimbo alioutoa hivi karibuni uitwao “No one like Oboma” akimwimbia rais wa Marekani Barrack Obama ni kwa mapenzi yake mwenyewe  kwa Rais huyo ambaye ameandika historia kwa mtu mweusi kutawala Taifa kubwa kama U.S. of A.

Kuhusiana na swala ilo la Dokii kumuimbia Obama nyimbo alifunguka hivi: Nimeguswa sana na Rais Obama nikiwa kama msanii na mwenye mapenzi na Afrika nikaguswa na harakati za mtu mweusi kutawala Taifa kubwa kama Marekani huku nikikumbuka hotuba za mwanaharakati Martin Luther King Jnr. alisema I have a Dream .. We shall be judged not by the color of our skin but the content of our character! Kauli hiyo imetimia kwa mtu mweusi kutalawa Marekani,”.

Na kuhusu  swala zima la Filamu nchini Actress huyo toka kwenye kiwanda cha Swahiliwood anasema kuwa kwa sasa anaandika filamu za kimapinduzi ambazo anatarajia hali ya filamu ikiwa shwari ataanza kuzirekodi ikiwa ni mchango wake kwa jamii husika kwani  anaamini kuna mahitaji mengi ya elimu kwa vijana lakini wanakosa elimu, Dokii pia alishawahi kumtungia wimbo wa pongezi Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Hii ndio video ya Wimbo wa Dokii aliomuimbia Barack Obama:


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!