Wednesday, September 26, 2012

PAH ONE WAKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUKUTWA NA SILAHA KWENYE LOCATION YA MOVIE


So apparently pamoja na kufanya muziki kundi la Pah One limeamua kufanya movie tena action!! Bahati mbaya wakati wa pilikapilika za kushoot filamu hiyo pande za Sinza, Dar es Salaaam, polisi waliwaotea na kuwakuta na vya moto (silaha).

Cha kufurahisha ni kuwa kumbe silaha hizo hazikuwa real, ni toys!!! Hata hivyo haikuwa rahisi kuwashawishi polisi kuwaachia kirahisi kwakuwa ilibidi waende kituo cha polisi kwanza ambako baada ya maelezo marefu mno, jamaa wakatolewa kwa dhamana, ikimaanisha kuwa bado wana msala na polisi!! 

Huenda Pah One hawajui taratibu za kuigiza filamu kama hizo ambazo mara nyingi waigizaji huomba vibali mapema kwa mamlaka husika ambazo huwa na taarifa mapema.

Next time Pah One mnataka kushoot filamu za kigangster ili kuonesha uhalisia wa mtaani, inabidi mpitie procedures zote za utumiaji wa location kutoka kwa mamlaka husika lasivyo yatawakuta mengine tena. 

Pah One ni kundi linaloundwa na wavulana watatu, Ola, Igwee na Nah Reel pamoja na msichana moja Aika.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!