Sunday, September 16, 2012

PRODUCER MANECKY AWAPIGA VIJEMBE WANAOMCHUKIA NA KUIPONDA STUDIO YAKE

Producer bora wa mwaka 2011-2012 kwenye tuzo za Kilimanjaro, Emmanuel Manecky ameamua kufunguka baada ya ‘haters’ wake wanamshambulia yeye na studio yake kuongezeka.

Kupitia Facebook, producer huyo aliyetengeneza hits kibao ukiwemo ‘Hakunaga’ wa Sumalee na ‘Mwaka Jana’ ya Izzo B jana aliandika:

“Habari nyingi zimekuwa zikisambaa hapa mjini hivi karibuni kuhusu Manecky and A.M Record..Sikuzote twajua kuwa kuna watu ambao hawapendi ona wengine waki advance to another level…..na hapo ndipo wanapo anza ongea mbovu, ili mradi tu uonekane mbaya mbele ya jamii na wote wanaokukubali.

Well,this is an official statement toka A.M Record and Manecky.
.
“Kwa wale wote wanaojaribu tuharibia jina,sisi hatuna kingine ila tu kusema kuwa mola ndiye atawalipa,sababu yeye ndiye aliyetufikisha hapa tulipo……..xo, sisi yetu ni kuendelea make hit songs na kupeleka mziki wetu katika level nyingine”…y’all have a nice weekend.


Hata hivyo hakuweza kuelezea kwa kina habari mbaya zinazosambazwa kuhusu yeye na studio yake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!