Friday, September 14, 2012

QUICK ROCKA AJIPANGA KUFUNGUA STUDIO NA RECORD LABEL YAKE


Rapper wa kundi la Rockers, Abbott Charles aka Quick Rocker amesema anaanzisha record label yake aliyoipa jina la 255.


Rapper huyo anayetamba na ‘club banger’ yake mpya iitwayo ‘Katika’ alisema pia anafungua studio yake ya kurekodi muziki aliyoipa jina la ‘Big Step’.

Akiongea na kipindi cha Block 4 Teen cha Down Town TV (DTV) weekend iliyopita, Quick alidai kuwa studio yake itapatikana maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo hitmaker huyo wa ‘Bullet’ alisema pamoja na kuwa na studio yake mwenyewe, bado ataendelea kufanya kazi na studio zingine na kila aina ya producer ilimradi apate kitu kizuri.


Akiongelea wimbo wake mpya, ‘Katika’, Quick Rocker alieleza kuwa aliamua kutoka tofauti kwakuwa muziki wa Tanzania umebadilika ambapo watu wengi hupenda nyimbo zinazochezeka.

Katika mahojiano hayo, rapper huyo alizungumzia pia uwepo wa kundi lake la Rockers ambalo lilikuwa limevunjika na kudai kuwa kundi hilo limerudi tena na mashabiki wategemee mambo mapya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!