Sunday, September 9, 2012

RAILA ODINGA AZIDI KUWATEKA WASANII MAARUFU WA KENYAWaziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga ameamua kujiweka karibu zaidi na wasanii maarufu nchini ambao huenda wakamsaidia kwenye kampeni za uchaguzi ujao nchini humo.

Baada ya kukutana na Prezzo na Jaguar mwezi uliopita, waziri huyo mkuu hivi karibuni amekutana pia na staa wa dancehall nchini humo,Redsun.


Haijulikani ni nini ambacho huzungumzwa kwenye mikutano hiyo, lakini wengi wanaamini kuwa huenda akawatumia wasanii hao kwenye kampeni yake ya urais wa Kenya.

Tayari kuna tetesi kuwa wanasiasa kadhaa wanafanya mazungumzo na Jaguar ili wautumie wimbo wake uitwao ‘Matapeli’ kwenye kampeni zao na huenda Raila Odinga akawa ni mmoja wao.

Uchaguzi wa urais nchini Kenya utafanyika mwezi March, 2013.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!