Monday, October 1, 2012

RICK ROSS NA YOUNG JEEZY WARUSHIANA RISASI KATIKA BET HIP HOP AWARDS 2012

Siku chache zijazo,msanii/Rapper Rick Ross,anatarajiwa kutua nchini Tanzania kwa ajili ya Fiesta 2012 ambayo waandaaji chini ya udhamini wa Serengeti Breweries wameiita Fiesta Bhaaas. 

Lakini wakati Rapper huyo kibonge kupindukia hajatua Bongo,tayari anaonyesha kile ambacho baadhi ya watu  wamewahi kizungumzia hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kwamba sio “role model” mzuri kwa vijana wa kitanzania kiasi kwamba wengi wanahoji imekuwaje waandaaji wa Fiesta wakaona yeye ndio anafaa!

 Ni hela tu au kuna haja pia ya kuwaletea vijana wa kitanzania wasanii ambao wana maadili fulani.

Katika usiku wa kurekodi utoaji wa tuzo za  BET Hip Hop kwa mwaka 2012 ambazo bado hazijarushwa katika luninga,Rapper huyo na Rapper mwingine Young Jeezy waliachiana matusi na baadaye kuzusha varangati ambalo lilipelekea polisi kuitwa kwani hewani risasi zilishaachiwa na tafrani ilikuwa kubwa kiasi kwamba nusura itishie utoaji mzima wa tuzo hizo ambao ulikuwa unaendelea.

 TMZ.COM wamefanikiwa kupata clip ya jinsi varangati hilo lilivyokuwa.Itazame hapa
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!