Sunday, September 9, 2012

RIHANNA ATEMA MVUA YA MATUSI KWA DRAKE NA YOUNG MONEYInaonekana mvua ya habari za Rihanna haitaki kukatika. Baada tu ya kusababisha bonge la issue kwa kumbusu mpenzi wake wa zamani, Chris Brown, sasa limeibuka lingine kubwa.

Wakati Drake na timu yake ya Young Money ilipopanda juzi jukwaani kwenye za MTV VMA’s kupokea tuzo ya Best Hip Hop video, camera zilizoom sura ya Rihanna na kumkuta akiongea maneno yaliyotafsirika kama “I hate these a**holes.”


Kuna tetesi pia kuwa Rihanna na Nicki Minaj walitupiana maneno kwenye tuzo hizo.

Hata hivyo baada tu ya show hiyo Rihanna alichukua private jet na kuelekea jijini London kwenye mambo yake.

Rihanna, Jay-Z na kundi la Coldplay watatumbuiza kwenye ufungwaji wa mashindano ya Paralympics.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!