Tuesday, September 11, 2012

SIMBA YAIGONGA AZAM 3-2, YATWAA NGAO YA JAMII


TIMU ya Simba SC leo imetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuilaza Azam FC kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Mpaka mapumziko, Azam FC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1, mabao yaliyowekwa kimiani na John Bocco na Kipre Tchetche wakati la Simba likifungwa kwa penati na Mghana Daniel Akuffo.

 Simba walijipatia ushindi katika kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wao hatari, Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto. Mpaka mwisho wa mchezo Simba 3, Azam FC 2.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!