Thursday, September 20, 2012

SKENDO ZASABABISHA AUNT LULU APORWE BWANA


MREMBO aliyetambulika kwa jina la Fatma Mchina ambaye huko nyuma alikuwa aolewe na Tevez amekiri yeye ndiye aliyemnyang’anya bwana Kimwana Manywele 2006, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Akipiga  stori na mpekuzi wetu siku chache baada ya kuripotiwa kwenye gazeti kuwa demu huyo na Aunty Lulu wamegombania pedeshee, Fatma alifunguka kuwa ni kweli amemnyang’anya Aunty bwana’ake lakini akasema na si pedeshee.


“Nilipoachana  na Tevez, nilinasa kwa Bond bin Salim, ni kweli alikuwa mchumba’ake, lakini alikuja kwangu baada ya kuchoshwa na vituko vya Aunty Lulu, sasa namshangaa anataka vita na mimi, anajisumbua tu haniwezi kwa lolote,” alisema Fatma.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!