Tuesday, September 11, 2012

SUMA LEE NA LINEX WAUNGANA KUFANYA KOLABO MOJAWasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya almaarufu kama Bongo fleva juzi usiku walikwenda mpaka Kibaha mkoani pwani katika Studio za Usanii Production na kufanya kolabo ambayo ilichukua zaidi ya masaa manne kukamilika na kupewa jina la Boda Boda.


Kolabo hiyo ambayo imesimamiwa na Produza mahiri Fundi Samweli na wasanii hao wawili wenye staili mbili tofauti inasemekana kuwa itakapotoka itakuwa kali sana baada ya wadau waliokuwepo wakati kolabo hiyo ikifanyika kutonya kwamba ina viwango vya juu kwani wasanii wote wawili wamejitahidi kufunikana kuanzia sauti, utunzi na ujumbe.


“Kaka shughulu ilikuwa pevu studio kwani wasanii wote wawili walifika studio mida ya jioni na kuanza kujipanga kwa takriban masaa mawili baada ya hapo walienda ndani na kuanza matayarisho ya mwisho kabla ya kuingiza sauti mida ya usiku sana". Tunamnukuu mdau  John Anthony aliyekuwepo maeneo ya studio siku ya jumatatu jioni mpaka usiku
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!