Sunday, September 30, 2012

TAFF YAJIPANGA KUANZA KUTOA ADHABU KWA WAIGIZAJI WANAOVUNJA MAADILI YA KITANZANIASHIRIKISHO la filamu Tanzania TAFF, limetoa tamko kwa wasanii wake hasa wale wanaoendelea kufanya vitendo vya uvunjaji wa maandili kuwa wanasuburi sheria kutoka BASATA, ili waaze kuchukua hatua za kinidhamu.

Akizungumza na mtandao huu
,Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba, alidai kuwa wanasikitishwa na tabia ambazo zinanaendelea kufanywa na wasanii wake kwani vitendo hivyo vinawafanya hata wadau wa tasnia hiyo kuounguza kasi ya kununua kabisa filamu zao zinapotoka.

“Sisi kama TAFF tunasuburi sheria kutoka BASATA, acha waendelee kujiachia na tabia zao chafu, kwani baada ya sheria hii kutoka watakuwa matumbo joto na hatutafanya mchezo tutahukumu kila anayevunja sheria na kanuni,”
alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa sheria ambayo wanaisuburi kutoka BASATA ni ile ambayo itakuwa inatoa adhabu kwa wasanii ambao wanavunja maandili, kanuni zitakazojieleza ndani ya sheria hiyo na wengi wote ambao wataonekama kwenda kinyume.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!