Saturday, September 8, 2012

TAMTHILIA YA JUMBA LA DHAHABU KUREJEA KWENYE TV TENA KUPITIA TBC1


Tamthilia ya Jumba la Dhahabu iliyowahi kutamba nchini inatarajiwa kurudi tena kwenye TV baada ya kusimama kwa muda mrefu.

Muongozaji wa tamthilia hiyo Tuesday Kihangala maarufu kwa jina la Mr. Chuzi, amesema wameamua kuja na Season 2 ya Jumba la Dhahabu kutokana na maombi ya mashabiki wa tamthilia hiyo nchini.


Jumba la Dhahabu ndio tamthilia iliyowapa majina wasanii kama Mzee Chilo, Mr. Chuzi na Miriam Jolwa anayejulikana zaidi kama Jini Kabula.

Mr. Chuzi amesema Season 2 ya tamthilia hiyo itakayotayarishwa na kampuni ya Tuesday Entertainment Ltd itakuwa ikiruka mara tano kwa wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kupitia TBC1.
Miriam Jolwa - Jini Kabula Mr Chuzi Mzee Chilo

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!