Sunday, September 9, 2012

TANZANIA YAKAMA NAFASI YA 21 AFRIKA KWA USHINDANI WA KIUCHUMI, 120 DUNIANI KATI YA 144


Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) juzi lilitoa ripoti ya yake ya Global Competitiveness 2012-2013, ambayo iliyalinganisha mataifa katika hali ya ushindani kiuchumi.

Katika nchini 144 zilizolinganishwa, 38 ni za Afrika lakini ni Afrika Kusini, Mauritius, Rwanda na Morocco tu ndizo zilizoshika nafasi katika nusu ya kwanza ya orodha hiyo.

WEF inalitafsiri neno ‘competitiveness’ kama “mkusanyiko wa asasi, sera, na mambo yanayopima uzalishaji katika nchi.

Kiwango cha uzalishaji huonesha kiwango cha utajiri unaoweza kupatikana kwenye nchi.

Kiwango cha uzalishaji pia huainisha kiasi cha marejesho yanayopatikana kutoka kwenye kitega uchumi katika nchi.

Kutambua rank hizi, nchi ziliangaliwa katika nguzo 12 ambazo ni asasi zilizopo, miundo mbinu, mazingira ya biashara ndogo, afya na elimu ya msingi, elimu ya juu na mafunzo, ubora wa soko la bidhaa, ubora wa soko la ajira, maendeleo ya soko la kifedha, utayari wa kitechnolojia, size ya soko,  ubora wa biashara na uvumbuzi.

Orodha ya nchi za Afrika kwenye ripoti hiyo

Nchi
Nafasi barani Afrika
Nafasi Duniani 2012 – 2013 (kati ya nchi 144 duniani)
Afrika Kusini
1
52
Mauritius
2
54
Rwanda
3
63
Morocco
4
70
Seychelles
5
76
Botswana
6
79
Namibia
7
92
Gambia
8
98
Gabon
9
99
Zambia
10
102
Ghana
11
103
Kenya
12
106
Misri
13
117
Algeria
14
110
Liberia
15
111
Cameron
16
112
Libya
17
113
Nigeria
18
115
Senegal
19
117
Benin
20
119
Tanzania
21
120
Ethiopia
22
121
Cape Verde
23
122
Uganda
24
123
Mali
25
128
Malawi
26
129
Madagascar
27
130
Ivory Coast
28
131
Zimbabwe
29
132
Burkina Faso
30
133
Mauritania
31
134
Swaziland
32
135
Lesotho
33
137
Msumbuji
34
138
Chad
35
139
Guinea
36
141
Sierra Leone
37
143
Burundi
38
144

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!